top of page
Search

Anguko La Kinara Wa Azimio Raila Odinga

Editorial

By Simon Gilisho

Raila Odinga aliyeshindwa kunyakua kiti cha mwenyekiti AUC
Raila Odinga aliyeshindwa kunyakua kiti cha mwenyekiti AUC

Baada ya uamuzi wa dhati wa Raila Odinga kuzamia kwenye hatamu za kisiasa za kuwania uwenyekiti wa chama cha African Union Commission (AUC),nia na azma ya kukata kiu ya kisiasa ili kufaidi bara la Afrika kwa ujumla.Kinara wa Azimio akihamasisha kuwa taifa la Afrika linahitaji kujitegemea kwa kuegemea rasilmali za nchi zao bila matumizi ya mikopo ya mataifa ya nje.


Pilkapilka za Raila Odinga kugombea uwenyekiti chama cha AUC ilipigwa jeki na Mheshimiwa rais William Samoei Ruto,ili kufanikisha safari yake ya uwenyekiti wa bara la Afrika.Hata hivyo,mambo hayakwenda shwari kama ilivyokuwa matarajio ya wengi kwani mtumbwi wa uliobeba bahati yake ya uongozi huo ulitia kitumbua mchangani.


Anguko hili latokana na hatua ya jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) kumuidhinisha mpinzani wao,jambo ambalo dhahiri shahiri liliuguza donda  ndugu kwa Raila Odinga,kwa kuwa mataifa kumi na sita ya bara la Afrika yaligeuka kutomuunga Odinga mkono kwenye kinyang'anyiro hicho cha uwenyekiti wa chama AUC.

Hatimaye Odinga alisalimu amri baada ya Kiongozi kutoka taifa la Djibouti,Mahmoud Youssuf kumpiku kwa kumshinda kwa kura nyingi kwa awamu ya nne na sita mtawalia.Aidha Odinga aliridhika na matokeo hayo ya uchaguzi na kumpongeza mshindi, ama kweli asiyekubali kushindwa si mshindani.


Anguko hili la Odinga liliibuwa hisia mseto kwa Wakenya tofauti baadhi yao wakisema kuwa kufeli kwake kwenye kinyang'anyiro hicho cha uwenyekiti ni thibitisho ya yeye kurejea nchini tena kuwania kiti cha urais ifikapo mnamo mwaka wa 2027, hata hivyo wengine wana mtamzamo tofauti kuwa hakujaliwa kipaji cha uongozi kamwe!Michanganyiko hizi za hisia zilichipuka maeneo tofauti nchini hususan eneo la Kondele kaunti ya Kisumu ambapo matarajio ya wafuasi wa Odinga katika eneo yalikuwa ya kupigiwa mfano ila matarajio hayo yaligeuka kuwa matamanio.


Hofu nchini yaonekana kushamiri kote kwani matumaini ya Odinga kutaka kuwania kiti cha urais inatabiriwa. Takwimu zikionyesha kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa upande wa  Raila kufuatilia nyota yake ya mwisho kuelekea lango la ikulu ya rais iwapo litajifunguwa ifikapo kipindi hicho cha uchaguzi mkuu.Anguko hili la Odinga limeonekana kuwa pigo kubwa kwa Rais William Ruto kwani upinzani mkubwa kati ya viongozi hawa wawili unaonekana kuzibua mwanya wa ushindani mkali zaidi kwa uchaguzi unaosubiriwa kwa shaka na shauku.Hata hivyo,swali ambalo sasa linabakiya kujibiwa akilini mwa wakenya ni je,Odinga bado ana kiu ya kuwa rais nchini au la?

 

Hata hivyo ,Odinga baada ya uchaguzi huo wa kugombea uwenyekiti kumalizika alieleza kinagaubaga kwamba atarejea maskani yake  nchini Kenya,kisa na maana ana majukumu chungu nzima ya kutekeleza.Isitoshe Odinga aliongeza na kusema ataendelea kujitolea mhanga kwa shughuli zozote za ujenzi wa bara la Afrika pasi na kutozingatia poromoko lake la kujaribia nafasi ya uwenyekiti jijini Addis Ababa.

 

 

 

Mitazamo mbalimbali sasa yanakumbatiwa na wakenya wa azazi tofauti kutokana na anguko hili la Odinga kwa kuwa wanakosa imani na yeye jambo ambalo linaonekana kuzusha hadhi ya Raila Odinga kwa azma yake ya kukalia kigoda cha uongozi nchini ya kuwa rais licha ya kuwa ndoto yake ya kuwa mwenyekiti wa chama cha AUC kugonga mwamba.Fauka ya hayo,asillimia kubwa ya wakenya wamepoteza hamu kuu ya kumuunga mkono endapo atagombea kiti cha urais kwa awamu ya pili.Ila swali gumu linaloibuka ni je,Odinga atafanikiwa kwa kipindi hiki kingine cha pili au la?

 

Hata hivyo Rais William Ruto ameonekana kujawa na ukimya usiokuwa wa kawaida baada ya Odinga kula mwata kwa uongozi huo wa uwenyekiti jijini Addis Ababa,Ethiopia .Hii ikiwa ni sababu moja wapo inayothibitisha tishio kuu kwa Rais William Ruto kwa kampeni zake za kuwania urais mnamo kipindi hicho cha mwaka wa 2027.Swali ambalo litazalia kuwa kumbukumbu mawazoni mwa wakenya ni je ,anguko hili la Odinga litaleta manufaa kemkem au masaibu tele kwa wakenya?Ama anguko hili ni hatima ya Raila Odinga kufikia kikomo ya kutamani wadhifa wa urais nchini Kenya.

0 comments

Comments


bottom of page